Ezra 2Telezesha kushoto au kulia kubadili sura1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:3wazao wa Paroshi 2,1724wazao wa Shefatia 3725wazao wa Ara 7756wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,8127wazao wa Elamu 1,2548wazao wa Zatu 9459wazao wa Zakai 76010wazao wa Bani 64211wazao wa Bebai 62312wazao wa Azgadi 1,22213wazao wa Adonikamu 66614wazao wa Bigwai 2,05615wazao wa Adini 45416wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 9817wazao wa Besai 32318wazao wa Yora 11219wazao wa Hashumu 22320wazao wa Gibari 9521watu wa Bethlehemu 12322watu wa Netofa 5623watu wa Anathothi 12824watu wa Azmawethi 4225wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 74326wazao wa Rama na Geba 62127watu wa Mikmashi 12228watu wa Betheli na Ai 22329wazao wa Nebo 5230wazao wa Magbishi 15631wazao wa Elamu ile ingine 1,25432wazao wa Harimu 32033wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 72534wazao wa Yeriko 34535wazao wa Senaa 3,63036Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 97337wazao wa Imeri 1,05238wazao wa Pashuri 1,24739wazao wa Harimu 1,01740Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 7441Waimbaji: wazao wa Asafu 12842Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao wa // Shalumu, Ateri, Talmoni, // Akubu, Hatita na Shobai 13943Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,49wazao wa Uza, Pasea, Besai,50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,54wazao wa Nesia na Hatifa.55Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.58Watumishi wa Hekalu wote na // wazao wa watumishi // wa Solomoni 39259Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:60wazao wa // Delaya, Tobia na Nekoda 65261Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;65tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.66Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,67ngamia 435 na punda 6,720.68Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.