Yoshua 12Telezesha kushoto au kulia kubadili sura1Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.5Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.6Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.7Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:8nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):9mfalme wa Yeriko mmoja mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja10mfalme wa Yerusalemu mmoja mfalme wa Hebroni mmoja11mfalme wa Yarmuthi mmoja mfalme wa Lakishi mmoja12mfalme wa Egloni mmoja mfalme wa Gezeri mmoja13mfalme wa Debiri mmoja mfalme wa Gederi mmoja14mfalme wa Horma mmoja mfalme wa Aradi mmoja15mfalme wa Libna mmoja mfalme wa Adulamu mmoja16mfalme wa Makeda mmoja mfalme wa Betheli mmoja17mfalme wa Tapua mmoja mfalme wa Heferi mmoja18mfalme wa Afeki mmoja mfalme wa Lasharoni mmoja19mfalme wa Madoni mmoja mfalme wa Hazori mmoja20mfalme wa Shimron-Meroni mmoja mfalme wa Akishafu mmoja21mfalme wa Taanaki mmoja mfalme wa Megido mmoja22mfalme wa Kedeshi mmoja mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja23mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmoja mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja24mfalme wa Tirsa mmoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.