Zaburi 93Telezesha kushoto au kulia kubadili sura1Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele.3Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu.5Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.