Zaburi 96Telezesha kushoto au kulia kubadili sura1Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote.2Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.3Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.4Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.5Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu.6Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.7Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.8Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake.9Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake.10Katikati ya mataifa semeni, “ Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu.11Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;12mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;13itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.