Zaburi 128Telezesha kushoto au kulia kubadili sura1Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake.2Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.5Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.