Zaburi 129Telezesha kushoto au kulia kubadili sura1Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”